Q CHILLAR AFUNGUKA MAMBO MAKUU MATATU JUU JUU YA BIFU LA DIAMOND NA ALIKIBA
.
Tumepata bahati ya kufanya mahojiano na Q Chief na haya ndio mahojiano yetu na Q Chief
Mwandishi : kwa sasa katika mziki wa BongoFlava kumekua kuna fitini nyingi wakati mwingine wasanii kwa wasanii wanachonganishwa na mwisho wa siku unakua ugomvi, kwa mfano sasa hivi bifu la Ali Kiba na Diamond. Je Q Chie unalizungumziaje hili?
Q Chief : Yote wanayopitia ni changamoto ambazo pengine hawakuwahi kuzania kwamba watapitia. Mi nmepitia situation ambazo zimenijenga kua sugu na Legendary ndio maana ya kua mkongwe unapitia situation ambazo watu wengine wanakufosi ufike huko. Hata kama upo level fulani wanakushusha kwa kufikiria kwamba wanaweza kukushusha. unapandishwa na watu, unapandishwa na mwenyezi Mungu, unashushwa na watu, unashushwa na mwenyezi Mungu. Mfano nimekua nikiangalia Fiesta kwenye TV sikwenda kwa sababu nlikua na mambo yangu Studio, hakuna kitu kigeni nlichokiona, nmeona msanii wa marekani anafunikwa na msanii wa Tanzania ambaye ni Ali Kiba. Nmeona Ali Kiba ambaye amekaa kimya kwa miaka mitatu bila Airtime na watu wamemzungumzia vibaya, vizuri na nini wamemkubali tena. Ikiwa ni mtu yule yule ambaye wamemkataa na wakumuweka mtu mwingine juu. Hakuna kitu kisichowezekana, matokeo uliyoyaona juzi ndio matokeo yanayotokea na yataendelea kutokea. Hakuna Mungu wa hii kazi, hakunaga mfalme wa hii kazi ila kuna masultan wa Hii Kazi.