Pata Habari Motomoto za Nje na Ndani ya Nchi kwa njia ya E-mail, Andika E-mail yako hapo chini.


Home » » KWELI DIAMOND KIPENZI CHA WATU DAH

KWELI DIAMOND KIPENZI CHA WATU DAH

MAMA MMOJA NA WANAFUNZI WA CHUO WAANDAMANA KISA,DIAMOND KUZOMEWA LEADERS



Mama mmoja aitwaye Mariam Mustapha maarufu kama ‘’Mama Dangote’’mkazi wa Kimara,jijini Dar mfanyabiashara maeneo ya chuo cha Ustawi wa Jamii,ameandamana na wanafunzi wa chuo hicho baada staa wa Bongo Fleva,Diamond Platinumz kuzomewa kwenye tamasha la ‪#‎Serengetifiesta2014‬ pande za Leaders Club,Kinondoni Jumamosi hii.
Mama huyo akizungumza na Uheard ya xxl na Makorokocho Soudy Brown amesema anaumwa kwa sasa na amekosa raha tangu siku hiyo ya tamasha hilo ndiyo maana ameamua kuandamana ili kutoa dukuduku lake na kwamba waliofanya tukio hilo hawakufanya kitu kizuri.
‘’Nampenda sana Diamond na kiukweli nilisikitika sana Diamond kuzomewa alikosa raha sana hadi hakupafomu vizuri jukwaani hadi sasa mimi naumwa’’alisema Mama Dangote.
Aidha mama huyo alimtuhumu Ally Kiba kupanga watu wamzomee Diamond,akijibu tuhuma hizo mdogo wa Ali Kiba,Abdul Kiba alisema kuwa hawawezi kufanya kitu hicho,na hawajawalipa watu pesa ili kumzomeee Diamond.
 

Copyright © 2013. UBUYU KITAANI - Haki zote zimehifadhiwa
Template Modify by Habarizetuleo TEAM
Proudly powered by MAN DUGX