HIVI NDIVYO WEMA SEPETU ANVOPONDA MALI NCHINI CHINA
WAKATI
bebi wake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akiugulia maumivu ya
kuzomewa na mamia ya mashabiki wa muziki katika Tamasha la Fiesta
jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wikiendi iliyopita, Wema Sepetu
‘Madam’ anaponda raha ya maisha nchini China, Amani lina full data.
Chanzo
makini kilicho ‘kloz’ na muigizaji huyo nyota wa filamu nchini,
kimesema Wema alipaa na ndege ya Emirates wiki iliyopita, siku chache
kabla ya Tamasha la Fiesta, akiwa ameandamana na wanaume wawili, ambao
ni meneja wake, Martin Kadinda na Petit Man, wote wakiwa wamekaa daraja
la kwanza la dege hilo.
Chanzo
hicho kilizidi kunyetisha kuwa gharama zote za safari hiyo zilibebwa
na Madam mwenyewe na kwamba baada ya kufika katika jiji la Guangzhou
nchini humo, Wema na wanaume hao wawili walichukua vyumba katika Hoteli
ya Holiday Inn, inayotajwa kuwa moja ya hoteli ghali zaidi huko China.
“Yaani
Wema jamani ana mambo, inavyoonekana lile rhumba la wakati ule
ameshalisahau, amesahau kabisa kama alishafulia, sasa Mungu kamjaalia
kapata pesa anavyoitapanya ovyo mpaka roho inauma. Wewe fikiria mtu
amekwenda kuchukua vifaa vya biashara, unakwenda na hao wanaume wa kazi
gani kama siyo kupoteza fedha tu,” kilisema chanzo hicho.
Wema Sepetu ‘Madam’ akipozi.
Inadaiwa
kwamba kilichompeleka Wema katika nchi hiyo yenye watu wengi zaidi
kuliko yoyote duniani, ni ununuzi wa vipodozi, kwani ana mpango wa
kufungua duka kubwa katika eneo ambalo halijatajwa jijini Dar es
Salaam.
Baada
ya kufika huko, chanzo kinasema kuwa watu hao watatu wamekuwa wakiishi
maisha ya starehe, wakila bata katika klabu mbalimbali za usiku,
ambako wanajichanganya na watanzania wengine kuponda raha.