HUYU MISS NI MUONGO NA HII AIBU KAIBEBA LUNDENGA...
Jana mwandaaji wa mashindano hayo Lundenga aliitsha mkutano na waandishi wa habari na kutoa ufafanuzi ya kua mshindi huyo hana miaka 18 kama watu wanavyosema na kuweka vithibitisho ya kua Sitti ana miaka 23 kama cheti chake kinavyosema. Uongo ambao nauona hapa tumedanganywa ni kuhusu hicho cheti ambacho mimi nakiona ni feki ni kua kilitengenezwa mda mfupi kabla ya kuanza mashindano huku cheti cha kwanza ambacho ndicho kilichotumika kutengeneza hadi Passport yake inayoonyesha kua kazaliwa mwaka 1989 kikiwa kimepotea.
Na alipoulizwa kilivyopotea ulienda kutoa taarifa kituo gani cha polisi aligoma kutaja. Kwa nini agome na wakati ilikua rahisi tu kutaja jina la kituo cha polisi kama kweli alienda kutoa taarifa?? ni maswali mengi aliulizwa lakini akagoma hii ni dalili kua miss Tanzania wetu ni magumashi matupu. Haiwezekani mtu tunayemwamini akaiwakilishe Tanzania katika mashindano ya dunia ashindwe kujibu maswali muhimu kabisa kuhusu umri wake.
Hii ni aibu kubwa kwa Lundenga na nahisi atakua amejifunza kitu na hatarudia kupitisha mamiss kimagumashi hivi, na naamini hata yeye roho inamuuma kwa alichokifanya.
Unaweza tazama video ya mahojiano hayo hapa chini :
Imeandikwa na Eddie Sucre