JE BIFU LA SHILOLE NA SNURA MAJAMGA LIMEISHA NA SHILOLE KUIBUKA MSHINDI...?!
Mwaka mmoja nyuma mpinzani mkubwa wa Shilole alikua Snura aka mama wa majanga kama mwenyewe anavyojiita. Inasemekana hapo mwanzo Snura na Shilole walikua marafiki kipindi wakiigiza pamoja ila walikuja kukosana baada ya wote wawili kuanza kuimba. Bifu hilo lilifikia pabaya zaidi ikawa hawaongeleshani nakumbuka kuna kipindi iliandaliwa show Dodoma na ilitakiwa wote wafanye show siku moja Shilole akaamua kuikacha show hiyo kisa Snura alikuepo.
Kwa sasa Shilole anafanya vizuri sana kwani anapata show nyingi sana kwa hapa Dar na hata huko mikoani, huku Snura akiwa kimya kabisa. Swali ni kubwa je huu ndio mwisho wa Snura??? Je tatizo linalomfanya awe kimya kwa mda mrefu hivyo ni lipi??? Je tatizo ni yeye au ni uongozi unaomsimamia?? tunafanya kila njia kumtafuta meneja wa Snura aje kutusaidia kujibu maswali haya.