APIGWA RISASI MCHANA KWEUPE, MAGOMENI JIJINI DAR ES SALAAM
Mtu
asiyefahamika akiwa ndani ya gari lake mara baada ya kupigwa risasi
tumboni. Kushoto kwake ni mwanamke aliyekuwa naye garini.
...hawa jamaa nao waligongana, mwendesha pikipiki na mwenye gari katika eneo la tukio na kuanza 'kuzikunja'.
Mtu
mmoja ambaye hakuweza kujulikana jina lake mara moja amepigwa risasi
na watu wanaodhaniwa kuwa majambazi na kuporwa mkoba uliyokuwa garini
ambao haukujulikana ulikuwa na nini ndani yake. Tukio hilo limetokea leo
majira ya mchana maeneo ya Magomeni Mikumi jirani na kwa Sheikh Yahaya
jijini Dar es Salaam. Mtu huyo alipigwa risasi tumboni akiwa kwenye
gari yake Toyota Mark II (GX 100) yenye namba za usajili T487 AZW.
Kwenye gari hiyo, alikuwemo mwanamke mmoja akiwa amekaa kwenye kiti cha
mbele cha abiria ambaye hakujeruhiwa.