BAIKOKO MBONA CHA MTOTO!!..........+18
DUNIA IMEKWISHA ONAAA
APIGWA RISASI MCHANA KWEUPE, MAGOMENI JIJINI DAR ES SALAAM
Mtu
asiyefahamika akiwa ndani ya gari lake mara baada ya kupigwa risasi
tumboni. Kushoto kwake ni mwanamke aliyekuwa naye garini.
...hawa jamaa nao waligongana, mwendesha pikipiki na mwenye gari katika eneo la tukio na kuanza 'kuzikunja'.
Mtu
mmoja ambaye hakuweza kujulikana jina lake mara moja amepigwa risasi
na watu wanaodhaniwa kuwa majambazi na kuporwa mkoba uliyokuwa garini
ambao haukujulikana ulikuwa na nini ndani yake. Tukio hilo limetokea leo
majira ya mchana maeneo ya Magomeni Mikumi jirani na kwa Sheikh Yahaya
jijini Dar es Salaam. Mtu huyo alipigwa risasi tumboni akiwa kwenye
gari yake Toyota Mark II (GX 100) yenye namba za usajili T487 AZW.
Kwenye gari hiyo, alikuwemo mwanamke mmoja akiwa amekaa kwenye kiti cha
mbele cha abiria ambaye hakujeruhiwa.
KWELI DIAMOND KIPENZI CHA WATU DAH
MAMA MMOJA NA WANAFUNZI WA CHUO WAANDAMANA KISA,DIAMOND KUZOMEWA LEADERS
Mama mmoja aitwaye Mariam Mustapha maarufu kama ‘’Mama Dangote’’mkazi wa Kimara,jijini Dar mfanyabiashara maeneo ya chuo cha Ustawi wa Jamii,ameandamana na wanafunzi wa chuo hicho baada staa wa Bongo Fleva,Diamond Platinumz kuzomewa kwenye tamasha la #Serengetifiesta2014 pande za Leaders Club,Kinondoni Jumamosi hii.
Mama huyo akizungumza na Uheard ya xxl na Makorokocho Soudy Brown amesema anaumwa kwa sasa na amekosa raha tangu siku hiyo ya tamasha hilo ndiyo maana ameamua kuandamana ili kutoa dukuduku lake na kwamba waliofanya tukio hilo hawakufanya kitu kizuri.
‘’Nampenda sana Diamond na
kiukweli nilisikitika sana Diamond kuzomewa alikosa raha sana hadi
hakupafomu vizuri jukwaani hadi sasa mimi naumwa’’alisema Mama Dangote.
Aidha mama huyo alimtuhumu Ally Kiba kupanga watu wamzomee Diamond,akijibu tuhuma hizo mdogo wa Ali Kiba,Abdul Kiba alisema kuwa hawawezi kufanya kitu hicho,na hawajawalipa watu pesa ili kumzomeee Diamond.
Aidha mama huyo alimtuhumu Ally Kiba kupanga watu wamzomee Diamond,akijibu tuhuma hizo mdogo wa Ali Kiba,Abdul Kiba alisema kuwa hawawezi kufanya kitu hicho,na hawajawalipa watu pesa ili kumzomeee Diamond.
MAMBO MAKUU MATATU JUU JUU YA BIFU LA DIAMOND NA ALIKIBA
Q CHILLAR AFUNGUKA MAMBO MAKUU MATATU JUU JUU YA BIFU LA DIAMOND NA ALIKIBA
.
Tumepata bahati ya kufanya mahojiano na Q Chief na haya ndio mahojiano yetu na Q Chief
Mwandishi : kwa sasa katika mziki wa BongoFlava kumekua kuna fitini nyingi wakati mwingine wasanii kwa wasanii wanachonganishwa na mwisho wa siku unakua ugomvi, kwa mfano sasa hivi bifu la Ali Kiba na Diamond. Je Q Chie unalizungumziaje hili?
Q Chief : Yote wanayopitia ni changamoto ambazo pengine hawakuwahi kuzania kwamba watapitia. Mi nmepitia situation ambazo zimenijenga kua sugu na Legendary ndio maana ya kua mkongwe unapitia situation ambazo watu wengine wanakufosi ufike huko. Hata kama upo level fulani wanakushusha kwa kufikiria kwamba wanaweza kukushusha. unapandishwa na watu, unapandishwa na mwenyezi Mungu, unashushwa na watu, unashushwa na mwenyezi Mungu. Mfano nimekua nikiangalia Fiesta kwenye TV sikwenda kwa sababu nlikua na mambo yangu Studio, hakuna kitu kigeni nlichokiona, nmeona msanii wa marekani anafunikwa na msanii wa Tanzania ambaye ni Ali Kiba. Nmeona Ali Kiba ambaye amekaa kimya kwa miaka mitatu bila Airtime na watu wamemzungumzia vibaya, vizuri na nini wamemkubali tena. Ikiwa ni mtu yule yule ambaye wamemkataa na wakumuweka mtu mwingine juu. Hakuna kitu kisichowezekana, matokeo uliyoyaona juzi ndio matokeo yanayotokea na yataendelea kutokea. Hakuna Mungu wa hii kazi, hakunaga mfalme wa hii kazi ila kuna masultan wa Hii Kazi.