Staa
wa filamu Bongo, Lulu Semagongo ‘Aunt Lulu’ amefunguka kuwa skendo ya
kujihusisha ya vitendo vya kisagaji inayomuandama imemsababishia msala
mkubwa kwa mama yake na kuamua kumuomba radhi.
Akizungumza
na paparazi wetu, Aunty Lulu alisema mama yake ana ugonjwa wa presha
hivyo amejirekebisha katika eneo hilo ili asiweze kumkwaza tena mzazi
wake huyo.
“Najua
nimemuumiza sana mama yangu, nachukua fursa hii kumuomba sana samahani
kwa kuwa najua aliumia sana kutokana na habari hiyo lakini nataka
kumuambia kuwa mimi mtoto na nitaendelea kuwa mwanaye, anisamehe mama
yangu,” alisema Aunty Lulu.