Pata Habari Motomoto za Nje na Ndani ya Nchi kwa njia ya E-mail, Andika E-mail yako hapo chini.


Home » » SOMA HII AUNT EZEKIEL ANACHOFANYA!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

SOMA HII AUNT EZEKIEL ANACHOFANYA!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!


Baada ya penzi la staa wa Bongo Movies, Aunt Ezekiel Grayson na dansa wa Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Moses Iyobo ‘Moze’ kushamiri kwa kasi ya umeme, wawili hao wamenaswa wakisindikizana kimalovee kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar.
Staa wa Bongo Movies, Aunt Ezekiel Grayson akiwa na dansa wa Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Moses Iyobo ‘Moze’ wakielekea uwanja wa ndege.
Tukio hilo lililopigwa chabo na mwanahabari wetu mwanzo mwisho, lilijiri Ijumaa iliyopita ambapo wawili hao walionekana wakiingia pamoja kimahaba eneo hilo.
Aunt Ezekiel na Moses Iyobo wakiagana kwa mabusu uwanja wa ndege.
Aunt ambaye ni mke halali wa Sunday Demonte anayedaiwa kufungwa Uarabuni kwa msala wa madawa ya kulevya, alionekana na Iyobo ambaye pia ni mume wa mtu (Mwengy) wakishikana mikono katika sehemu ya kukagulia mizigo kisha wakaagana kwa mabusu motomoto.
Aunt Ezekiel akipozi kwenye kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar.
Mwanahabari wetu alipomuuliza Aunt kulikoni, alifunguka: “Nakwenda Marekani lakini wengine wote unaowaona wananisindikiza kama desturi ya watu kusindikizana.”
 

Copyright © 2013. UBUYU KITAANI - Haki zote zimehifadhiwa
Template Modify by Habarizetuleo TEAM
Proudly powered by MAN DUGX