Ni
tamaa ya ngono au ni nini? Hivyo ndivyo unavyoweza kujiuliza baada ya
kubainika kwamba mastaa watatu Bongo, Wema Isaac Sepetu, mpenzi wake
Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na Aunt Ezekiel Grayson wanatajwa kwenye
mchepuko hatari wa kuzungukana kimalovee, Ijumaa lina kila sababu ya
kukujuza.
Ishu hiyo imebumburuka baada ya hivi karibuni mastaa kutengeneza vichwa vya habari kila kukicha kuhusiana na mambo yao hayo.
AUNT NA MOZE IYOBO
Duru za kihabari zinaonesha kwamba hivi karibuni mwigizaji Aunt, bila ya kupepesa macho huku akijua dhahiri kuwa ni mke wa mtu, Sunday Demonte alifungua kinywa na kuapa kuwa hawezi kuachana na mume wa mtu, Moses Peter Iyobo ‘Moze Iyobo’ ambaye ni densa wa Diamond.
Aunt alitamka maneno hayo akijua fika kuwa Moze Iyobo ni mume wa mwanamke aitwaye Mwengy ambapo wanaishi Mbagala jijini Dar, wakiwa wamejaliwa mtoto mmoja.
“Dah! Natambua kuwa msanii ni kioo cha jamii lakini si kwa Aunt, hana hadhi ya kuitwa kioo cha jamii kutokana na tabia yake ya kuchepuka wakati ni mwanandoa,” alidai mmoja wa watu wake wa karibu.
Mdau mwingine wa sanaa za nyumbani aliyejitambulisha kwa jina la Said, mkazi wa Mwananyamala jijini Dar, alimshangaa Aunt kukiri hadharani kuwa ana uhusiano usiofaa na Moze Iyobo ambaye ni shemeji wa Wema kwa Diamond na yeye (Aunt) ni shosti wa Wema.
Alisema kwamba, kwa hadhi yake, Aunt hakupaswa kutoa kauli hiyo ili watu waendelee na minong’ono kuhusiana na yeye (Aunt) tofauti na alivyofunguka bila aibu ukizingatia ni mke wa mtu.
“Unajua kwa nini nasema Aunt anajidhalilisha au anawadhalilisha wanawake wenzake ni pale anapokiri kuwa ndoa yake ipo tena bado anampenda mumewe huku anakuja kusema kuwa anampenda Moze Iyobo, huo kama siyo mchepuko ni nini?” alihoji Said.
Uchunguzi ulionesha kwamba, huku wakijua kila kitu waliwaruhusu Ahmed Hashim ‘Petit Man’ (Toto ya Wema) na Esma Platnumz ‘kuchepuka’ huku Petit akiwa ni shemeji wa Diamond kwa Wema.
Pia Diamond alifanya ‘misteki’ kumuacha mdogo wake, Esma ‘kuruka’ na Petit kwa kuwa ni shemeji yake.
KAJALA ANAINGIAJE?
Ilibainika pia kwamba Petit aliwahi kuchepuka na mwigizaji Kajala Masanja ‘Kay’ ambaye ni mke wa mtu, Faraji Agostino aliyeko gerezani na hilo likiwa wazi hata kwa hao akina Wema na Diamond.
“Hebu jaribu kuangalia huo mzunguko na mkanganyiko uliopo hapo. Yaani ni aibu tosha,” alisema mdau mwingine kuhusiana na ishu hiyo.
Hivi karibuni kwenye Viwanja vya Leaders, Kinondoni jijini Dar, Mwenyekiti wa Klabu ya Bongo Movie Unity, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ aliwavaa mastaa hao na kuanika aibu yao huku akimshutumu Aunt ambaye alifika maeneo hayo akiwa ameongozana na mpenzi wake huyo wa sasa, Moze Iyobo.
Steve alisikika akimwambia Aunt kuwa hamtendei haki Moze Iyobo na anamnyima uhuru mkubwa kutokana na umri wake ambao anaweza hata kumzaa.
“Unajua wewe Aunt unastahili kuwa na mtoto mkubwa mwenye umri usiokuwa tofauti na huyu Moze Iyobo.“Hivi kwa nini unajidhalilisha kiasi hicho kwani wazee wenzako hujawaona hadi kumbemenda mtoto wa watu?” alisika Steve akimpasha Aunt kwa sauti ya juu.
Akiendelea kumpasha Aunt, jamaa huyo alikwenda mbali zaidi pale alipomwambia Aunt kwamba anahisi kuwa uhusiano wake na Moze Iyobo ni sharti kutoka kwa Diamond kumpa Wema ili alifanyie kazi na kumwambia kuwa ahakikishe yeye (Aunt) anakuwa na Moze na Petit Man amuoe Esma.
“Unajua hivi karibuni baada ya Diamond kuandika yale maneno katika Mtandao wa Instagram, nilisikia waliachana sasa naona Diamond alimwambia Wema kama unataka nikurudie ahakikishe kuwa wewe Aunt unakuwa na huyu mtoto (Moze Iyobo) halafu yule dogo mwenye rasta sijui mnamuita Petit Man ahakikishe anamuoa Esma dada yake Diamond,” alisema Steve.
Baada ya Steve kutoa dukuduku lake mwigizaji huyo aligeuka mbogo na kumwambia Steve kuwa amuache kwa raha zake kwani anampenda Moze Iyobo hata aseme nini hawezi kumuacha.
“Hata uongee nini Steve, siwezi kumuacha mpenzi wangu, nampenda sana na hayo masharti unayoyasema kuwa ameyatoa Diamond unayajua wewe, niachie nile raha zangu na Moze wangu,” alisema Aunt akimwangushia Moze Iyobo bonge la ‘kisi’.
KUTOKA IJUMAA
Ni kweli wasanii ni kioo cha jamii lakini kwa kuwa wamekuwa ‘vichwa ngumu’ kutenda yale yanayowafanya kuwa vioo vya jamii ni vema jamii yenyewe ikachuja mema na kuyachukua kisha kuwaacha wabaki na hayo machafu yao.
Mastaa
watatu Bongo, Wema Isaac Sepetu, mpenzi wake Nasibu Abdul ‘Diamond
Platnumz’ na Aunt Ezekiel wakiwa katika picha ya pamoja.
KILA KUKICHAIshu hiyo imebumburuka baada ya hivi karibuni mastaa kutengeneza vichwa vya habari kila kukicha kuhusiana na mambo yao hayo.
AUNT NA MOZE IYOBO
Duru za kihabari zinaonesha kwamba hivi karibuni mwigizaji Aunt, bila ya kupepesa macho huku akijua dhahiri kuwa ni mke wa mtu, Sunday Demonte alifungua kinywa na kuapa kuwa hawezi kuachana na mume wa mtu, Moses Peter Iyobo ‘Moze Iyobo’ ambaye ni densa wa Diamond.
Aunt alitamka maneno hayo akijua fika kuwa Moze Iyobo ni mume wa mwanamke aitwaye Mwengy ambapo wanaishi Mbagala jijini Dar, wakiwa wamejaliwa mtoto mmoja.
Mume wa mtu, Moses Peter Iyobo ‘Moze Iyobo’ akiwa na ‘Diamond Platnumz’.
AUNT KIOO CHA JAMII?“Dah! Natambua kuwa msanii ni kioo cha jamii lakini si kwa Aunt, hana hadhi ya kuitwa kioo cha jamii kutokana na tabia yake ya kuchepuka wakati ni mwanandoa,” alidai mmoja wa watu wake wa karibu.
Mdau mwingine wa sanaa za nyumbani aliyejitambulisha kwa jina la Said, mkazi wa Mwananyamala jijini Dar, alimshangaa Aunt kukiri hadharani kuwa ana uhusiano usiofaa na Moze Iyobo ambaye ni shemeji wa Wema kwa Diamond na yeye (Aunt) ni shosti wa Wema.
Alisema kwamba, kwa hadhi yake, Aunt hakupaswa kutoa kauli hiyo ili watu waendelee na minong’ono kuhusiana na yeye (Aunt) tofauti na alivyofunguka bila aibu ukizingatia ni mke wa mtu.
“Unajua kwa nini nasema Aunt anajidhalilisha au anawadhalilisha wanawake wenzake ni pale anapokiri kuwa ndoa yake ipo tena bado anampenda mumewe huku anakuja kusema kuwa anampenda Moze Iyobo, huo kama siyo mchepuko ni nini?” alihoji Said.
‘Moze Iyobo’ akiwa na familia yake.
WEMA NA DIAMONDUchunguzi ulionesha kwamba, huku wakijua kila kitu waliwaruhusu Ahmed Hashim ‘Petit Man’ (Toto ya Wema) na Esma Platnumz ‘kuchepuka’ huku Petit akiwa ni shemeji wa Diamond kwa Wema.
Pia Diamond alifanya ‘misteki’ kumuacha mdogo wake, Esma ‘kuruka’ na Petit kwa kuwa ni shemeji yake.
KAJALA ANAINGIAJE?
Ilibainika pia kwamba Petit aliwahi kuchepuka na mwigizaji Kajala Masanja ‘Kay’ ambaye ni mke wa mtu, Faraji Agostino aliyeko gerezani na hilo likiwa wazi hata kwa hao akina Wema na Diamond.
“Hebu jaribu kuangalia huo mzunguko na mkanganyiko uliopo hapo. Yaani ni aibu tosha,” alisema mdau mwingine kuhusiana na ishu hiyo.
'Petit Man' akipozi kimahaba na Kajala Masanja, 'K'.
STEVE NYERERE AANIKA AIBU YAOHivi karibuni kwenye Viwanja vya Leaders, Kinondoni jijini Dar, Mwenyekiti wa Klabu ya Bongo Movie Unity, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ aliwavaa mastaa hao na kuanika aibu yao huku akimshutumu Aunt ambaye alifika maeneo hayo akiwa ameongozana na mpenzi wake huyo wa sasa, Moze Iyobo.
Steve alisikika akimwambia Aunt kuwa hamtendei haki Moze Iyobo na anamnyima uhuru mkubwa kutokana na umri wake ambao anaweza hata kumzaa.
“Unajua wewe Aunt unastahili kuwa na mtoto mkubwa mwenye umri usiokuwa tofauti na huyu Moze Iyobo.“Hivi kwa nini unajidhalilisha kiasi hicho kwani wazee wenzako hujawaona hadi kumbemenda mtoto wa watu?” alisika Steve akimpasha Aunt kwa sauti ya juu.
'Petit Man' yule yule akiwa na dada yake 'Diamond Platinum', Esma.
NI SHARTI LA DIAMOND KWA WEMAAkiendelea kumpasha Aunt, jamaa huyo alikwenda mbali zaidi pale alipomwambia Aunt kwamba anahisi kuwa uhusiano wake na Moze Iyobo ni sharti kutoka kwa Diamond kumpa Wema ili alifanyie kazi na kumwambia kuwa ahakikishe yeye (Aunt) anakuwa na Moze na Petit Man amuoe Esma.
“Unajua hivi karibuni baada ya Diamond kuandika yale maneno katika Mtandao wa Instagram, nilisikia waliachana sasa naona Diamond alimwambia Wema kama unataka nikurudie ahakikishe kuwa wewe Aunt unakuwa na huyu mtoto (Moze Iyobo) halafu yule dogo mwenye rasta sijui mnamuita Petit Man ahakikishe anamuoa Esma dada yake Diamond,” alisema Steve.
Mwenyekiti wa Klabu ya Bongo Movie Unity, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ akifafanua jambo.
AUNT AWA MBOGOBaada ya Steve kutoa dukuduku lake mwigizaji huyo aligeuka mbogo na kumwambia Steve kuwa amuache kwa raha zake kwani anampenda Moze Iyobo hata aseme nini hawezi kumuacha.