MHE. MAGUFULI UPO?
WAKATI serikali ya awamu ya nne inayoongozwa na Rais Jakaya Kikwete ‘JK’ ikifanya kazi nzito ya kujenga barabara kwa gharama kubwa na kuzilinda kwa kuweka mizani ili kudhibiti magari yanayozidisha uzito, baadhi ya madereva wa mabasi wamekuwa wakikaidi kwa makusudi agizo hilo.
Uchunguzi
uliofanywa na mwandishi wa Oparesheni Fichua Maovu ‘OFM’, umebaini
kuwa, baadhi ya madereva wa mabasi hayo wamekuwa wakimpiga changa la
macho Waziri wa Ujenzi, John Magufuli anayesimamia barabara nchini.
Madereva
hao huzidisha abiria na hivyo basi kukosa sifa kwenye mizani wakati wa
ukaguzi lakini wanachofanya sasa, kila wanapokaribia mizani hupunguza
uzito kwa kuwashusha baadhi ya abiria nyuma ya mizani na baadaye
kuwapakia kwa mbele baada ya kupima.
Mwandishi
wetu alipokea taarifa toka kwa wananchi wema wanaolitakia maendeleo
taifa lao ambapo mwishoni mwa wiki iliyopita, paparazi wetu alifanya
uchungu na kubaini uwepo wa hujuma hizo za makusudi.
Basi moja linalofanya safari zake kati ya Moshi (Kilimanjaro) na Dar es Salaam (jina tunalo) lilinaswa likifanya mchezo huo kwenye mizani iliyopo jirani na Daraja la Wami.
Basi moja linalofanya safari zake kati ya Moshi (Kilimanjaro) na Dar es Salaam (jina tunalo) lilinaswa likifanya mchezo huo kwenye mizani iliyopo jirani na Daraja la Wami.
Dereva
wa basi hilo aliwashusha abiria zaidi ya watano ambao walitembea kwa
miguu hadi ng’ambo ya pili ya mizani hiyo na baada ya basi hilo kupima
uzito, kondakta aliwaita abiria hao kama anavyoonekana pichani na
kuwapakia tena.
Waziri
wa Ujenzi, Dkt. John Magufuli alipotafutwa na mwandishi wetu kuhusiana
na tukio hilo, simu yake haikupatikana. Jitihada zinaendelea.