DONGO:DIAMOND ATAKA WEMA AMZALIE MTOTO .....WEMA AKATAA KUOGOPA KUPOTEZA MVUTO NA UMAARUFU
Diamond Platnumz kwa muda sasa amekuwa akimwambia mpenzi wake Wema Sepetu abebe mimba kwasababu yeye anataka mtoto lakini Wema amekuwa mgumu kukubali kudungwa mimba na Diamond kwasasa kwa madai kuwa hayupo tayari kuzaa muda huu sababu ikiwa ni kuwa atapoteza mvuto wake kiumbo na pia kuchuja kiumaarufu, kitu ambacho hakitaki.
Chanzo kilicho karibu na Wema na Diamond kimeiambia Mpekuzi kuwa:
"Ni muda sasa Diamond anataka mtoto tatizo Wema hataki, anaogopa kushuka umaarufu na pia kupoteza umbo lake lenye mvuto.
"Kitendo
hicho kimemuweka njia panda Diamond kwa sababu pesa anayo ya kutosha
kulea mtoto ila haelewi kwanini Wema hataki wapate mtoto eti kwa
kisingizio cha kupoteza fame yake na umbo"
Hata
hivyo Diamond juzi kupitia akaunti zake za mitandao ya kijamii aliweka
post inayoshabihiana na maelezo ya chanzo hicho. Diamond ni kama alikuwa
amerusha Dongo hilo kwa Wema kwa kuandika ...
"Kwa
mtazamo wangu mimi naona kuzaa hakumfanyi mtu azeeke au awe wa
kizamani, ni tabia tu ya mtu mwenyewe.... na ndio maana dada zetu kama
Beyonce, Nancy sumary, Kim Kardashian na kadhalika wana watoto na still
wanafanya vizuri.....Au we mtazamo wako ukoje?........ "
Vile
vile mapema wiki hii gazeti moja la burudani liliandaka habari
inayokaribiana maana na hii kuwa Wema hataki kuzaa kuogopa kupoteza
mvuto wake na umaarufu