MANGE KIMAMBI ATOA DARSA LA BURE KWA WATANZANIA.
Haya ndio mambo tisa aliyo yasema Mange Kimambi kuhusu
i. Roho za Watanzania
ii. Wanawake wa Bongo Movie
iii. Wanawake wenye rangi nyeusi
iv. Ndoa
v. Michango ya harusi
vi. Asicho takiwa kukifanya mwanamke anaye tarajia kufunga ndoa na mwanaume wa kizungu
vii. sifa kuu ya mwanamke anaye stahili kupigwa ndoa.
viii. Mbuta Nanga,
Kwa ufupi katika maelezo yake, Mange Kimambi, ameongea mambo yafuatayo ,ambayo kiukweli yana ukweli mkubwa sana ndani yake.
1. KUHUSU ROHO ZA WATANZANIA:
Kuhusu roho za watanzania, Mange Kimambi anasema “ Hivi watanzania wakoje jamani?? roho mbaya kama mapaka meusi” Hapa Mange anasema watanzania wengi wana roho mbaya,na hawapendi kuona wenzao wakiwa wanafanikiwa. Ameenda mbali zaidi kwa kufananisha roho za watanzania na roho za mapaka meusi. Kama ulikuwa haufahamu katika ulimwengu wa
rohoni, paka mweusi huwa anawakilisha shetani mbaya.Mange anaweza
kuwa sahihi katika hili, ni kweli kabisa watanzania
wengi huwa hawapendani na hawapendi kuona watanzania wenzao wakiwa wanafanikiwa,iwe ni kwa hapa hapa Bongo au hata kwa Diasporas. WATANZANIA TUBADILIKE.
2. KUHUSU MAISHA YA WANAWAKE WA BONGO MOVIE : Kuhusu maisha ya wanawake wanao igiza bongo movie,Mange anasema
“ Eti wanamchambua sababu ni star wa bongo movie so angejua jinsi ya kuvaaa. Washenzi wakubwa nani
kawaambii kuwa bongo movie ndo kuwa na uwezo wa kuvaa? Bongo movie
hakuna lolote wala chochote ukiona mwanamke wa bongo movie anavaa vizuri
au anaishi vizuri ujue either ana biashara zake za pembeni au ana
mwanaume anamlea, bongo movie wanafaidika wahindi wanaosambaza hizo
movie “
Hapa Mange anasema wasanii wa kike wa Bongo movie,wengi wao hawana kipato chochote cha maana wanacho kipata kupitia filamu. Wanao faidika hapo ni wahindi ambao ndio wauzaji wa kazi za wasanii huku wasanii wakibaki na majina makubwa bila kipato chochote kinacho endana na majina yao pamoja na kazi zao.Matokeo yake wengi wao wanaamua kujiingiza katika biashara ya kuuza miili yao kwa wanaume ili wapate pesa za kujikimu.
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inapaswa kudhibiti wizi wa kazi za wasanii wa muziki na filamu Tanzania pamoja na kusimamia haki zao ili kuhakikisha wasanii hawa wanapata maslahi yanayo endana na ugumu wa kazi yao. Sanaa ni kazi kama zilivyo kazi nyingine, tasnia ya sanaa ikiwezeshwa basi inawezan kutengeneza maelfu ya ajira kwa vijana wa kitanzania na hivyo kuisaidia serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kupambana na tatizo la ukosefu wa ajira nchini.
3. KUHUSU WANAWAKE WENYE RANGI NYEUSI : Kuhusu wanawake wenye rangi nyeusi,Mange anasema wanawake wenye rangi nyeusi ( Wasio jichubua ) ndio wanawake wenye mvuto. Haina haja ya mwanamke kujichubua ili awena mvuto,msikiemwenyewe.
“
Kwanza huyu dada kawashindaje uzuriii, mweneywe alivyo black na ngozi
ya kutereza , mtoto portable shepu inaeleweka, wenyewe sasa isingekuwa
wana matiti yani usingejua kama ni wanaume au wanawake. “
4. KUHUSU NDOA :Mange Kimambi anasema ndoa ni jambo la heri sana na ni bahati kubwa sana kwa mwanamke kuolewa,so mwanamke anapopata bahati ya kuolewa anapaswa kupongezwa sana bila kujali kipato au hali ya kiuchumi ya mwanaume aliyemuoa na sio kuanza kumchamba nakumsema vibaya kama ambavyo baadhi ya wanawake walivyo fanya kwa mwanadada Lucy Komba. Msikie mwenyewe:
“ Mumuache huyu binti nyau nyie, mtu katoka kuolewa badala mumpe hongera mnamchambua utadhani aliwaomba mchango wa harusi?”
5. KUHUSU MICHANGO YA HARUSI : Mange anasema unapotaka kufanya harusi, angalia uwezo wako ukoje, usijilazimishe kufanya harusi ya gharama kubwa sana ambazo haziendani na uwezo wako. Mange anawaponda watu wenye kasumba ya kufanya harusi ya bei ghali kwakutegemea michango ya watu wakati wao wenyewe vipato vyao vipo chini,matokeo yake inakuwa kuanza kuwasumbua watu wengine kwa michango ya harusi.
Msikilize mwenyewe :
“
Si bora huyu kafanya harusi ya uwezo wake, mijitu mingine inataka kuvaa
nguo expensive kwa pesa za watu, michango ya harusi mnawadai watu
utadhani madeni, mfyuuuuuuuu, alafu mkifanya harusi kubwa mnabinua
matako eti ulifanya harusi nzuri. Ulifanya au watu walifanya? mfyuuuuu. “
6. KUHUSU ASICHO TAKIWA KUKIFANYA MWANAMKE ANAYE JIANDAA KUFUNGA NDOA NA MWANAUME WA KIZUNGU. Kama wewe ni mwanamke ambaye unatarajia kufunga ndoa na mwanaume wa kizungu,hutakiwi kabisa kuomba michango ya harusi. This is simply because,wazungu huwa hawaombi michango ya harusi,kwa
sababu harusi ni suala binafsi la mtu. Hayo si maneno
yangu,ni maneno ya MangeKimambi,msome mwenyewe hapo chini :
“ Wengine
mtuanaolewa na mzungu lakini bado anaomba michango ya harusi, how tacky
is that? Yani mpaka suti ya mzungu inatoka kwenye michango ya watu….”
7. KUHUSU SIFA YA MWANAMKE ANAYE STAHILI KUOLEWA: Mange anatoa ushauri kwa wanaume ambao bado hawajoa.Sifa kuu ya mwanamke anaye paswa kuolewa ni Yule asiye penda makuu.Ukio mwanamke mwenye kupenda makuu wafwaa!!!
“
Dada wa watu alivaa vile alivyopenda yeye na mume wake na hana makuu
,angekuwa mjinga kama nyie mnaomsema angeenda hata kukopa au kukodisha
nguo za maana ili awafurahishe,lakini ni mwanamke mwenye akili zake.”
8. KUHUSU MBUTA NANGA : Alicho kiandika hapa Mange naona ni kama dongo kwa Mbuta Nanga,kwa sababu ndio mwanamke maarufu Tz ambaye amewahi kuripotiwa kudaiwa kubakwa.
Na
hapo ni wivu tu maana asilimia kubwa ya wanaomchamba hawana hata
mabwana wa kusingizia, na kwa roho mbaya kama hizo za kutukana wanawake
wenzenu ambao hawajawakosea kitu mtaishia kubakwa tu…..
9. KUHUSU PEPO ANAYE WASABABISHIA WANAWAKE KUPATA NUKSI YA KUTOKUOLEWA:
Mange anasema,kuwa na chuki dhidi ya maendeleo na mafanikio ya watu wengine ni miongoni mwa mambo yanayo weza kuleta pepo la nuksi kwa wanawake.
“
Na hapo ni wivu tu maana asilimia kubwa ya wanaomchamba hawana hata
mabwana wa kusingizia, na kwa roho mbaya kama hizo za kutukana wanawake
wenzenu ambao hawajawakosea kitu mtaishia kubakwa tu…..Mnajitiaga nuksi
wenyewe.”
10. KUH USU WANAUME WAKIZUNGU: Mange Kimambi anasema usimjudge mwanaume wa kizungu kwa kumwangalia tu.
“
Au issue ni kuolewa na mzungu? mmemsema mzungu wa watu choka mbaya
sijui nini? hata kama si wake yeye, nyie umaskini wa huyo mzungu
unawahusu nini? na wazungu hamuwajui nyie anaweza tembea na soksi
zimetoboka kwenye account ana mamilinion….. usim judge mzungu kwa mavazi
hata siku moja “