MISS Tanzania 2014, Sitti Mtemvu juzi alilipua bobu la 2, baada ya kulazimisha safari ya kwenda kushiriki Miss World 2014 huku vigezo na masharti hasa yanayohusiana na cheti chake cha kuzaliwa yakipingana naye.
Pamoja na Lundenga kuweka wazi mchakato waliyotumia hadi kumfanya Sitti kuibuka na taji la Miss Tanzania 2014, bado kuna dosari za wazi ambazo zilijionesha kuwa mrembo huyo analazimisha safari hiyo kwani cheti chake cha kuzaliwa kinaonesha ana miaka 23 lakini namna cheti hicho kilivyotolewa ndiyo utata na ulazima ulipotokea.
Baadhi ya waandishi walimuhoji Sitti juu ya cheti hicho ambacho kinaonesha kimetolewa na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Uzamini (RITA), Septemba 9, mwaka huu, siku 32 tu kabla ya kutwaa taji hilo.
Swali ambalo lilitawala kwenye kikao hicho lilikuwa ni kwa nini cheti hicho kitoke ndani ya muda mfupi wakati anaonekana alikuwa akiishi nje ya nchi kwa muda mrefu, na kwamba huwezi kuishi nje ya nchi bila paspoti ambayo pia upatikanaji wake unatakiwa kuwa na cheti cha kuzaliwa alisema kilipotea!
Akaulizwa alitoa ripoti kituo gani cha polisi ili waandishi waende kuulizia, akagoma!
“Mimi nadhani alichoongea Hashim Lundenga kinajitosheleza na zaidi naona mnanisakamasakama bila sababu ya msingi, nimechoka kuandamwa na vyombo vya habari pamoja na mitandao.
“Kama kuna mtu anaona cheti hakiko sahihi basi aende ofisi husika ili ajiridhishe juu ya hilo hata suala la kuniambia nina mtoto nafikiri mnaweza kwenda hospitali yoyote kuulizia hilo,” alisema Sitti.
..amekaa pembeni ili aweze kumfafanulia japo kwa ufupi juu ya mkanganyiko huo kama tangu alipomzaa Sitti hakuwahi kumchukulia cheti cha kuzaliwa hadi alipoamua kushiriki mashindano hayo.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Lino International Agency ambao ni waratibu wakuu wa Mashindano ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga.
“Mambo
ya Sitti naomba muulize yeye maana ndiye mshiriki wa Miss Tanzania,
mimi sijawahi kushiriki hata siku moja na hapa nimekuja kumleta yeye
tu, hivyo siwezi kuzungumza lolote juu ya hilo, kikao hiki kimeandaliwa
na Miss Tanzania na si ukoo wa Mtemvu,” alisema mama huyo.Hili ni bomu la pili, la kwanza ni lile lwa kudai ana miaka 18 siku alipojitambulisha kwenye shindano hilo, Mlimani City, Dar na kuzua utata mkubwa kwenye jamii.