Mabosi huwatafutia safari kama njia ya kuwanasa kwa kuwa wanapokuwa
hotelini pekee, wanawake wengi wanakosa ujasili wa kukataa.Wengine hutoa
ofa kama vile kupandishwa vyeo,kununulia magari au hata safari za
nje.Wengi wanaofanya haya ni waume za watu, wengine ukitajiwa ni ngumu
kuamini kwa namna wanavyoonekana wana hekima usoni au mavaziyao.Licha ya
harakati mbalimbali za kumkomboa mwanamke, bado kuna mabosi nchini
wanawanyanyasa wanawake kwa kuwalazimisha kufanya nao ngono.Wapo
wanaonyanyaswa au hata kuteswa ikiwemo kusemwa maneno machafu au
kutishiwa kufukuzwa kazi kwa sababu tu wamekataa kutoa penzi kwa
bosi.Wale wanaokubali, wengine wanaishia kupewa ahadi hewa za
kufundishwa magari, kupelekewakozi mbalimbali. Hata hivyo mbaya zaidi ni
kwamba mabosi wengine hata kama wameoa, hupenda kuwamiliki wanawake hao
kana kwamba ni wake zao kwa kuwafuatilia sana nyendo zao.Ukahaba wa
mabosi hufanywaje?Baadhi ya wanaume kwa mwonekano ni vigumukuamini kama
ndiyo wanaofanya vitendo vichafu kwa wafanyakazi wao. Wanaposimama
kwenye vikao, utasema mtu huyu, lakini wafanyakazi wa kike wamekuwa ni
wenye kuwanyanyasa mno.Baadhi ya mabosi wamekuwa wakitoa vitisho kuwa
‘kama hunipi penzi nitakuporomosha cheoau hata kukufanyia visa vyovyote
hadi uhame’.Katika baadhi ya ofisi badala ya mabosi kutumika kama
washauri wa wafanyakazi wao kuzipenda ndoa na nyumba zao, ndio wamekuwa
wakitumia fedha zao kuwahonga wanawake hata magari, huku makatibu
muhtasi wakidaiwa kuwa ndio wanaosumbuliwa zaidi.Wapo mabosi huwaingia
wanawake wakiwemo wake za watu kwa kuwapangia safari za mikoani au nje
ya nchi hasa wanapoona hawana wepesi wa kukubaliana na matakwa
yao.“Nakumbuka kuna bosi mmoja katika ofisi moja nyeti aliwahi kudaiwa
kumnunulia gari mke wa mtu kabla ya kuhama chombo hicho,” anasema mkazi
mmoja wa Kimara.Bosi aliweza kumpa safari ya nje mwanamke nakisha
kumnunulia gari zuri kuliko la mumewe.Hii ni moja ya kati ya matukio
mengi ya mabosi kuwaingiza wafanyakazi wao katika ngono badala ya kuwa
ndio washauri wema kwa wafanyakazi ili waweze kuziheshimu ndoa zao.Sifa
zifaazo kwa mabosiKwa mujibu wa msomi maarufu katika tansia yauongozi,
Christopher Rocchio wa Marekani, katika chapisho lake la ‘Secret
Millionaire’, mabosi wanapaswa kutoa miongozo mizuri ya namna ya kuishi
vema ndani na nje ya sehemu za kazi, kwa bahati mbaya, baadhi yao
wamekuwa sababu ya kuharibika kwa ndoa za wafanyakazi wao.Wataalamu
wengine katika masuala ya uongozi na utawala, Ruth Faulkner katika
chapisho lake la “Viridor boss’ na Fernandez, Maria-Elena katika gazeti
la Los Angeles Times, mabosi wanaweza kuchangia kuharibu au kujenga
ndoaza wafanyakazi wao kutokana na mafundisho au namna wanavyoendesha
mambo sehemu za kazi.Je, wewe ni bosi wa namna gani au ofisini kwenu
mabosi wenu wakoje? Kila mtu aliyeko kwenye ajira analo jibu lake. Hata
hivyo kwa vyovyote inavyokuwa ni suala la msingi kila bosikutafakari
kwamba dhamana aliyonayo si kufanya ngono wala kutongoza wafanyakazi na
kuwatisha, bali kushirikiana nao kuongeza mafanikio katika eneo la
kazi.Simulizi ya mmoja wa wanawake Mwajuma Sabuni (sio jina lake
halisi), ni mfanyakazi katika kiwanda kimoja jijini Dar es Salaam (jina
linahifadhiwa) analalamikia unyanyasaji wa kijinsia kutoka kwa wenye
vyeo vya juu yao.“Nimefanya kazi katika kiwanda hiki kwa miaka saba
sasa. Sisi wafanyakazi wa kike imekuwa nikawaida kulazimishwa kufanya
ngono.Baadhi ya wasimamizi wa vitengo ndio wahusika wakuu wa kulazimisha
wapewe ngono, ukiwakataa ajira yako inakuwa hatarini”.Haya ni baadhi ya
mambo mabaya wanayofanyiwa wanawake sehemu za kazi.Baadhi yao
hulazimika kujiingiza kwenye ngono zisizo salama kwa sababu tu wanaogopa
kuwaambia mabosi wao watumia kinga kwa hofu kwamba itaonekana kama ni
kuwadhalilisha kuwa huenda wana Ukimwi. Katika mkutano wa wadau wa
kupambana na ugonjwa wa Ukimwi hivi karibuni jijini Dar es Salaam,
wanawake wako kwenye hatari zaidi yakuathirika na ugonjwa huo kwa sababu
baadhi ya hao mabosi hawatumii kinga na huwa hawako tayari kupima, kwa
bahati mbaya zaidi wale wanaofanya nao baadhi yao huogopa kuhoji
chochote hivyo mabosi hufanya watakavyo ikiwemo kutotumia
kinga.Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya kudhibiti Ukimwi nchini (Tacaids),
Dk Fatma Mrisho anasema, “Hatari ya wanawake kuathirika na Ukimwi ni
kubwa mno. Pia ni changamoto kubwa inayohitaji jitihada za kila mmoja
wetu.”Naibu Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini
(Tucta), Hezron Kaaya anapendekeza mifuko ya hifadhi ya jamii kuanzisha
mfuko wa kuwasaidia wanawake na wasichana.Mkurugenzi wa Sera na Utetezi
wa Chama cha Waajiri nchini (ATE), Justina Lyela ambaye amewataka
waajiri nchini kuepuka kuwapunja wafanyakazi wa kike ukilinganisha na
wanaumeili kuwawezesha kiuchumi.Tamwa na unyanyasajiChama cha Waandishi
wa Habari Wanawake (Tamwa), katika moja ya mpango mkakati wake wa miaka
mitano 2010-2014, pamoja na mambo mengine kimepanga kufanya shughuli
ambazo zitaimarisha elimu kwa mtoto wa kike kwa kupunguza vitendo vya
ukatili wa kijinsia.Unyanyasaji wa kijinsiaUnyanyasaji wa kijinsia ni
tendo baya kwa haki za binadamu na linasababisha maumivu kwa wahusika.
Vilevile, linahusisha kumlazimisha mtu kufanya nae mapenzi bila ridhaa
yake. Lakini kufanya mapenzi na watu kama baba, mama, kaka, dada, babu
au bibi ni aina nyingine ya unyanyasaji wa jinsia.Unyanyasaji wa
kijinsia ni kosa la jinai. Unyanyasaji huo ni pamoja na kutumia maneno
kwa mfano baadhi ya mabosi huwatishia wafanyakazi wa kike kwamba
wasipokubali kufanya nao ngono watawafukuza kazi.Unyanyasaji sio
unahusisha sauti, ishara au maonyesho ya sehemu za mwili kwa makusudi
kinyume na matakwa ya mtu, kwamba kwa mfano mtu anaweza kukuonyesha
sehemu za siri au kukuvamia kwa kugusa sehemu zako za siri kama njia ya
kukushawishi mfanye ngono.Kanuni za adhabu (sura ya 16) kama
zilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002, zipo wazi kwamba hakuna mtu
anayeruhusiwa kujamiiana na mtu mwingine bila ya ridhaa yakeĆ.anayefanya
hivi maana yake ni sawa na ubakaji.Ni kosa kupigwa busu bila
ridhaaSheria ziko wazi kuwa hakuna mtu anayeruhusiwa kushika viungo vya
siri vya uzazi, au kukupiga busu bila ya ridhaa ya mhusika.Hivi
karibuni, Tamwa ilizindua ripoti ya utafiti waunyanyasaji wa kijinsia
uliofanyika Aprili mwakahuu katika wilaya 10 za Tanzania Bara na
Zanzibar.Mkurugenzi wake, Valery Msoka anasema waafiti waliwahoji watu
mbalimbali katika ngazi za familia na kupata ukweli wa hali halisi ya
unyanyasaji wa kijinsia.W i l a y a zilizofanyiwa utafiti ni Wete (Pemba
Kaskazini), Mjini Magharibi (Unguja Magharibi), Unguja Kusini, Kisarawe
(Pwani), Newala (Mtwara), Mvomero (Morogoro), Lindi vijijini na Ruangwa
(Lindi), Kinondoni na Ilala, Dar es Salaam.Kwa mujibu wa Tamwa matendo
haya ya unyanyasaji wa kijinsia kwa ujumla yameshamiri nchini, na kwamba
zaidi ya asilimia 39 ya wanawake nchini wamekuwa wakifanyiwa vitendo
vya ukatili.Watuhumiwa wa unyanyasaji huu kwa kiwango kikubwa ni
wanaume, huku sheria zikionekana kushindwa kuchukua mkondo wake
ipasavyo.Mfano halisi ni ripoti ya Polisi Zanzibar, ambayoinasema katika
mwaka 2011, yalikuwapo matukio 268 ya unyanyasaji yaliyoripotiwa, kesi
zilizofikishwa mahakamani ni 55, hata hivyo ni kesi moja ndiyo iliyomtia
mtuhumiwa hatiani.Je, nini kifanyike kuepusha mateso wanayofanyiwa
wanawake maofisini? Ni changamoto ambayo inapaswa kuendelea kufanyiwa
kazi ili kuepusha mabosi viwembe wanaoendelea kuwanyanyasa wanawake
wakitumia madaraka yao.Waziri Sophia Simba wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia
na Watoto, ametaka kuwepo usawa wa fursa kama vile elimu na rasilimali
za uchumi hasa kwa wanawake.Waziri Simba anaamini kwamba kwa jitihada
ambazo Serikali inaendelea nazo nchini, tatizo launyanyasaji wa kijinsia
litaendelea kupungua.Baadhi ya mikakati hiyo ni pamoja na uwepo
washeria mbalimbali ambazo kwa namna moja ama nyingine zinaonekana
kushawishi watu kujali haki za kijinsia. Chanzo: Mabosi wanavyotumia
vyeo