Jennifer
Kyaka maarufu kwa jina la kisanii kama Odama, usiku wa kuamkia
Jumapili iliyopita alinaswa Live akiwa kwenye pozi la aina yake akiwa
na pedeshee maarufu jijini Dar anayefahamika kama Papaa Daudi ambaye
anadaiwa kuwa mume wa mtu.
Msanii nyota wa filamu za kibongo, Jennifer Kyaka Odama akiwa
kwenye pozi la kimahaba na anayedaiwa kuwa ni mume wa mtu.
Wawili
hao walinaswa wakiwa kwenye pozi hilo ndani ya Ukumbi wa Ten Lounge
uliopo Makumbusho jijini Dar es Salaam ambapo Odama alikuwa akimdekea
mwanaume huyo kama mtu wake wa karibu.
Wakiwa
ukumbini humo, wawili hao walionekana kupata kiburudisho kwa namna
yake huku mara kwa mara wakigonga ‘chiaz’ na kunyweshana mvinyo na
kuwafanya waliokuwa karibu yao kuwaonea gere.
Licha
ya macho ya watu kuonekana kuwatazama kwa muda mwingi, lakini wawili
hao hawakumjali mtu bali waliendelea kuponda raha huku mikono ya
mwanaume ikiwa haichezi mbali mapajani mwa Odama.
Baada
ya kupata picha kadhaa za wawili hao, Paparazi wetu aliwasogelea na
kuwauliza kama wao ni mtu na mwenza wake, lakini wakabeza na kumtaka
awaache wale raha zao.