Rapper Azma aachia wimbo unaofundisha wanaume kuwafikisha wapenzi wao kileleni......Video iko hapo chini

Rapper Azma Mponda ameamua kujitolea kupitia ngoma yake kuwafunda wanaume wenzake namna ya kuwafikisha wapenzi wao katika kilele cha raha wakati wa tendo maarufu zaidi duniani, ngono.
Akiongea , Azma amesema ameamua kuachia wimbo wake huo uitwao ‘Jinsi ya Kumkifikisha Mpenzi Wako Kileleni’, baada ya kuona amekuwa akifanya nyimbo zenye ujumbe wa kijamii kwa muda mrefu lakini watu wanazichukulia poa.

“Kikubwa nimeona nimefanya kazi nyingi sana zenye ujumbe mkubwa mfano ‘Mungu Inusuru Tanzania’, ‘Utata wa Katiba’, ‘Wanasubiri Nife’, ‘Kuwa na Azma’, ‘Kila Kitu Kila Siku’, ambayo nimerelease last week lakini ndo mapokeo yake ni madogo.
