PICHA A TUKIO IA:MADEE
Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva a.k.a Rais wa Manzese, Hamad Ally ‘Madee’ hivi karibuni alilala katika Kituo cha Polisi cha Kigamboni, Dar akihusishwa na utekaji wa dereva wa bodaboda, Suedi Waziri (pichani) kisha kumpa kipigo ambapo inadaiwa alisoteshwa kinomanoma.
Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva a.k.a Rais wa Manzese, Hamad Ally ‘Madee’ akiwa mikononi mwa Polisi
Baada
ya tukio hilo lililotokea mwishoni mwa wiki iliyopita, Ijumaa lilinasa
picha zinazomuonyesha msanii huyo akihenyeshwa kituoni hapo huku mmoja
wa watu wanaoishi karibu na eneo hilo akinyetisha kuwa, licha ya ustaa
wake Madee alikiona cha mtemakuni.
Dereva wa bodaboda, Suedi Waziri aliyetekwa na kushambuliwa na Madee.
“Mimi
nilikuwepo pale kituoni, nilimshuhudia akiwa amepigwa pingu huku
polisi kama sita hivi, mmoja akiwa na silaha wakiwa wamemuweka chini ya
ulinzi wakimpeleka mahakamani.“Alionekana aliyechoka sana huku akiwa
na hofu ila inavyodaiwa baadhi ya watu wake wa karibu walikuwa wakihaha
kumnusuru baada ya kulala selo,” kilidai chanzo hicho.
Majeraha ya mguuni aliyopata Suedi Waziri baada ya kushambuliwa na Madee.
Kufuatia
msala huo, msanii huyo alipandishwa kizimbani katika Mahakama ya
Kigamboni na baadaye kuwekewa dhamana na baba yake ambapo kesi yake
itatajwa tena Oktoba 6, mwaka huu.
Madee
anadaiwa kumteka Suedi na kwenda kumsulubu nyumbani kwake Manzese
baada ya kijana aliyekuwa amepakia kwenye bodaboda yake kukwapua simu
ya msanii huyo na kukimbia.