Pata Habari Motomoto za Nje na Ndani ya Nchi kwa njia ya E-mail, Andika E-mail yako hapo chini.


Home » » MKEEE ANAUMAAA!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

MKEEE ANAUMAAA!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!


Baba mmoja alietambulika kwa jina moja la Kaga mkazi wa Mwanga Kisangani ''B'' jirani na Saigoni amemuuwa mpenzi wake kwa kumnyonga nakumtumpa katika Makorongo ya Kilimahewa ''B'' Chini ya Shule ya Msingi Kilimahewa.

Taarifa za awali zinasema kulikuwa na ugomvi baina yao hao wapenzi wawili hali iliyopelekea mwanamke (Mama Koku) kumshtaki mwanaume Mahakamani na kusababisha Mwanaume kufungwa miezi miwili jera.
siku kadhaaa baada ya mwanaume kutoka gerezani alipata habari kuwa mpenzi wake huyo aliesababisha kuwekwa ndani anatembea na mwanaume mwingine ndipo mwanaume huyo alipopanga njama/namna ya kutekeleza mauwaji hayo.

taarifa zinasema mara baada ya mwanaume kudhamiria kutekeleza tukio hilo lililokinyume na neno la MUNGU katika kitabu kile cha Kutoka 20.13 alimwambia mpenzi wake kuwa leo nimejisikia tutoke out twende Beach za Gorden tukajivinjari,mwanamke (Mama Koku) bila shaka lolote aliongozana nae mpenzi wake huyo ndipo wakiwa njiani katika makorongo ya Kilimahewa ''B'' mwanaume alimbadilikia ghafla na kumkaba kooni mwanamke na kupelekea kupoteza maisha.

mara baada ya mwaume kufanya unyama huo inasemekana zilipita siku kadhaa ndipo mwanaume alipowapiga simu kwa ndugu wa mwanamke huyo...njoeni mchukue mzoga wenu....aliongea mwanaume huyo.
Mwanaume huyo anajishughulisha na shughuli za ubebaji mizigo katika soko kuu la Kigoma Mjini.


Mara baada ya mwanaume huyo muuwaji kutoa taarifa kwa ndugu wa marehemu,ndugu walifanya jitihada za kumtafuta ndugu yao ndipo walipoukuta mwili katika Makorongo ya Kilimahewa ukiwa umeharibika vibaya na walilazimika kuzika hapo hapo.

Jeshi la Polis mkoani Kigoma linaendelea kumtafuta mtuhumiwa na atakapo patikana atapelekwa katika vyombo vya sheria.

taaarifa hii imethibitishwa na Diwani wa kata ya Mwanga Kaskazini Mh.Fransic Mangapi
 

Copyright © 2013. UBUYU KITAANI - Haki zote zimehifadhiwa
Template Modify by Habarizetuleo TEAM
Proudly powered by MAN DUGX