Pata Habari Motomoto za Nje na Ndani ya Nchi kwa njia ya E-mail, Andika E-mail yako hapo chini.


Home » » job vacancies!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

job vacancies!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!






Licha ya kuonekana na madansa wa kike katika jukwaa la Fiesta 2014 Mwanza, Diamond anasema hajabahatika kumpata dansa wa kike mwenye vigezo anavyovitaka.“Sina madansa wa kike pale wawili ni wa Vanessa naweza sema wote si wangu, zamani nilikuwa na madansa wa kike, lakini kwa sasa Tanzania tuna upungufu kwenye muziki wa Bongo Fleva na muziki wa bendi kuna madansa ambao wamebobea kucheza muziki wa dansi pekee. Nilitamani kuwa na madansa wa kike zamani lakini ilishindikana maana kuwapata ni ngumu sana,” anasema na kuongeza: “Mpaka sasa bado natafuta madansa wa kike sijawapata, nahitaji dansa wa kike ambaye anajua, awe anajiamini afuatilie madansa wa nje wanachezaje, awe na unyamwezi kidogo ni ngumu sana, awe mbunifu afuatilie muziki wa nje na vitu kama hivyo. Kwa hiyo nikatamani nifanyaje nikaamua kuazima madansa wa watu nifanye nao shoo,” anasema. Akiwazungumzia madansa wake wa kiume ambao ni sita, Diamond anasema ni madansa wanaolipwa pesa ndefu ukilinganisha na madansa wote Afrika Mashariki.


"Siwezi kusema nawalipa kiasi gani itakuwa kama nawavua nguo, lakini hakuna madansa wanaolipwa vizuri kama wangu Afrika Mashariki, ikiwa bei inaongezeka na mimi nawaongeza katika malipo yao. Wako sita kwa kweli nimetoka nao mbali tangu ‘Kamwambie’ mwaka 2009, nimekua nao kifikra, kiumri na kiakili na kuona kwamba hawa ni mzigo wangu mimi na wanafanya kazi pamoja na mimi, wale ni mafanikio yangu wana msaada mkubwa sana pengine nisingekuwa hapa bila wao,” anasema. Hata hivyo, anaweka wazi kwamba linapofika suala la shoo za nje, huwa inategemea ni wapi kwani shoo zingine hairuhusiwi kwenda na madansa wote hivyo huwa anawabadilisha kwa zamu. Katika mahojiano hayo maalum na Mwananchi, superstar huyo alisema kuwa kwasasa muziki wa Bongofleva unakubalika nje ya nchi tofauti na zamani.
 

Copyright © 2013. UBUYU KITAANI - Haki zote zimehifadhiwa
Template Modify by Habarizetuleo TEAM
Proudly powered by MAN DUGX