
Taarifa ikufikie kwamba sexy lady wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amemnasa aliyekuwa meneja wa Wema Isaac Sepetu, Martin Kadinda ambaye ndiye atakuwa meneja wake kwa sasa.
Kadinda ambaye hivi karibuni alimwaga kibarua kwa Wema, alisema kwamba aliongozana na Lulu hotelini hapo kwa kuwa kulikuwa na Fainali ya Shindano la Miss Ilala, Dar, wakiwa ni mtu na meneja wake kama alivyokuwa kipindi yuko na Wema.
Kwa upande wa Lulu, alionekana kufurahia maneno hayo na kufanikiwa kumpata meneja huyo huku akiongezea kuwa amefarijika kuwa na meneja kama Kadinda.“Huyu ni meneja bora na siyo bora meneja kwa hiyo kama mtu anataka kufanya kazi na mimi, aanze kwa meneja wangu,” alisema Lulu.
Ukaribu wa Lulu na Kadinda ulianza kitambo hata kabla Kadinda hajafahamika kama ilivyo sasa.