Pata Habari Motomoto za Nje na Ndani ya Nchi kwa njia ya E-mail, Andika E-mail yako hapo chini.


Home » » DARASA LA BURE KWA WATANZANIA.

DARASA LA BURE KWA WATANZANIA.

MANGE KIMAMBI ATOA DARSA LA BURE KWA WATANZANIA.

 
Mange  Kimambi.

Haya ndio  mambo  tisa aliyo  yasema  Mange  Kimambi  kuhusu
i.                   Roho za  Watanzania
ii.                Wanawake  wa  Bongo  Movie
iii.             Wanawake  wenye  rangi  nyeusi
iv.             Ndoa
v.                Michango  ya  harusi
vi.             Asicho takiwa  kukifanya   mwanamke  anaye tarajia kufunga  ndoa  na  mwanaume  wa  kizungu
vii.          sifa  kuu  ya  mwanamke anaye  stahili kupigwa  ndoa.
viii.       Mbuta  Nanga,

Kwa  ufupi   katika  maelezo  yake,   Mange  Kimambi,ameongea  mambo  yafuatayo ,ambayo  kiukweli  yana ukweli  mkubwa  sana ndani  yake.
1.    KUHUSU     ROHO   ZA    WATANZANIA:
Kuhusu   roho  za  watanzania,Mange  Kimambi  anasema  “ Hivi watanzania wakoje jamani?? roho mbaya kama mapaka meusi”  Hapa  Mange  anasema  watanzania wengi wana  roho   mbaya,na hawapendi  kuona  wenzao  wakiwa wanafanikiwa. Ameenda mbali   zaidi   kwa kufananisha  roho za  watanzania  na  roho  za  mapaka  meusi.  Kama ulikuwa haufahamu   katika  ulimwengu  wa rohoni,  paka mweusi huwa anawakilisha shetani mbaya.Mange  anaweza kuwa sahihi  katika  hili, ni  kweli kabisa  watanzania wengi  huwa hawapendani na  hawapendi  kuona  watanzania  wenzao wakiwa wanafanikiwa,iwe  ni  kwa hapa  hapa Bongo au  hata kwa  Diasporas. WATANZANIA  TUBADILIKE.


2.    KUHUSU  MAISHA   YA  WANAWAKE  WA  BONGO MOVIE  :  Kuhusu  maisha  ya  wanawake  wanao  igiza  bongo movie,Mange anasema
“ Eti wanamchambua sababu ni star wa bongo  movie so angejua jinsi ya kuvaaa. Washenzi wakubwa nani kawaambii kuwa bongo movie ndo kuwa na uwezo wa kuvaa? Bongo movie hakuna lolote wala chochote ukiona mwanamke wa bongo movie anavaa vizuri au anaishi vizuri ujue either ana biashara zake za pembeni au ana mwanaume anamlea, bongo movie wanafaidika wahindi wanaosambaza hizo movie “
Hapa   Mange  anasema  wasanii  wa kike  wa Bongo movie,wengi  wao  hawana  kipato chochote   cha  maana wanacho  kipata  kupitia  filamu.  Wanao  faidika hapo ni  wahindi  ambao  ndio  wauzaji  wa  kazi  za wasanii  huku wasanii  wakibaki  na  majina  makubwa  bila  kipato chochote kinacho  endana  na  majina  yao   pamoja   na  kazi zao.Matokeo   yake  wengi  wao  wanaamua   kujiingiza  katika biashara  ya   kuuza  miili yao  kwa wanaume ili   wapate   pesa  za kujikimu.
Serikali  ya  Jamhuri ya Muungano  wa   Tanzania  inapaswa   kudhibiti   wizi  wa  kazi  za  wasanii  wa   muziki  na  filamu Tanzania  pamoja   na  kusimamia  haki  zao  ili kuhakikisha wasanii  hawa  wanapata maslahi   yanayo  endana  na   ugumu wa kazi  yao. Sanaa  ni  kazi kama  zilivyo   kazi  nyingine, tasnia ya  sanaa ikiwezeshwa   basi  inawezan  kutengeneza maelfu  ya ajira  kwa vijana  wa  kitanzania  na hivyo  kuisaidia serikali   ya  Jamhuri   ya  Muungano  wa Tanzania  katika kupambana na  tatizo   la  ukosefu   wa ajira  nchini.



3.    KUHUSU     WANAWAKE    WENYE  RANGI  NYEUSI  : Kuhusu  wanawake wenye  rangi  nyeusi,Mange anasema  wanawake  wenye  rangi  nyeusi (  Wasio jichubua )  ndio wanawake wenye  mvuto.  Haina  haja  ya  mwanamke  kujichubua  ili awena mvuto,msikiemwenyewe.
“ Kwanza huyu dada kawashindaje uzuriii, mweneywe alivyo black na ngozi ya kutereza , mtoto portable shepu inaeleweka, wenyewe sasa isingekuwa wana matiti yani usingejua kama ni wanaume au wanawake. “

4.    KUHUSU  NDOA :Mange  Kimambi   anasema  ndoa ni jambo la heri  sana na ni  bahati  kubwa  sana  kwa  mwanamke  kuolewa,so  mwanamke  anapopata  bahati  ya  kuolewa  anapaswa   kupongezwa sana  bila   kujali  kipato  au  hali   ya  kiuchumi  ya  mwanaume aliyemuoa  na  sio kuanza  kumchamba  nakumsema vibaya  kama ambavyo  baadhi  ya  wanawake   walivyo  fanya  kwa mwanadada  Lucy  Komba.  Msikie mwenyewe:

“ Mumuache huyu binti nyau nyie, mtu katoka kuolewa badala mumpe hongera mnamchambua utadhani aliwaomba mchango wa harusi?”
5.    KUHUSU  MICHANGO   YA  HARUSI  : Mange  anasema unapotaka  kufanya  harusi,angalia uwezo  wako ukoje,usijilazimishe kufanya  harusi  ya gharama  kubwa sana ambazo  haziendani  na  uwezo  wako.  Mange anawaponda  watu  wenye  kasumba  ya  kufanya  harusi  ya bei  ghali  kwakutegemea  michango  ya  watu  wakati  wao wenyewe  vipato  vyao  vipo  chini,matokeo yake  inakuwa kuanza kuwasumbua  watu wengine  kwa  michango  ya harusi.
Msikilize  mwenyewe :
“ Si bora huyu kafanya harusi ya uwezo wake, mijitu mingine inataka kuvaa nguo expensive kwa pesa za watu, michango ya harusi mnawadai watu utadhani madeni, mfyuuuuuuuu, alafu mkifanya harusi kubwa mnabinua matako eti ulifanya harusi nzuri. Ulifanya au watu walifanya? mfyuuuuu. “

6.    KUHUSU  ASICHO  TAKIWA  KUKIFANYA  MWANAMKE ANAYE  JIANDAA  KUFUNGA  NDOA NA  MWANAUME  WA  KIZUNGU.  Kama  wewe  ni  mwanamke   ambaye   unatarajia   kufunga  ndoa na  mwanaume  wa kizungu,hutakiwi  kabisa  kuomba  michango  ya  harusi.This is  simply because,wazungu  huwa  hawaombi  michango  ya harusi,kwa sababu  harusi  ni  suala binafsi  la  mtu. Hayo  si maneno yangu,ni  maneno  ya MangeKimambi,msome mwenyewe   hapo   chini :
 Wengine mtuanaolewa na mzungu lakini bado anaomba michango ya harusi, how tacky is that? Yani mpaka suti ya mzungu inatoka kwenye michango ya watu….”

7.    KUHUSU   SIFA   YA  MWANAMKE  ANAYE  STAHILI KUOLEWA:  Mange  anatoa  ushauri  kwa  wanaume ambao bado  hawajoa.Sifa  kuu  ya  mwanamke anaye paswa  kuolewa  ni  Yule  asiye  penda  makuu.Ukio mwanamke  mwenye  kupenda  makuu  wafwaa!!!
“ Dada wa watu alivaa vile alivyopenda yeye na mume wake  na hana makuu ,angekuwa mjinga kama nyie mnaomsema angeenda hata kukopa au kukodisha  nguo za maana ili awafurahishe,lakini ni mwanamke mwenye akili zake.”
8.    KUHUSU  MBUTA  NANGA :  Alicho  kiandika  hapa Mange  naona ni kama  dongo   kwa  Mbuta  Nanga,kwa sababu  ndio  mwanamke  maarufu  Tz  ambaye  amewahi kuripotiwa   kudaiwa  kubakwa.
Na hapo ni wivu tu maana asilimia kubwa ya wanaomchamba hawana hata mabwana wa kusingizia, na kwa roho mbaya kama hizo za kutukana wanawake wenzenu ambao hawajawakosea kitu mtaishia kubakwa tu…..
9.    KUHUSU  PEPO  ANAYE  WASABABISHIA WANAWAKE  KUPATA  NUKSI  YA KUTOKUOLEWA:
Mange  anasema,kuwa  na  chuki  dhidi  ya  maendeleo  na mafanikio  ya  watu  wengine  ni  miongoni  mwa   mambo yanayo  weza  kuleta  pepo  la nuksi kwa  wanawake.
“ Na hapo ni wivu tu maana asilimia kubwa ya wanaomchamba hawana hata mabwana wa kusingizia, na kwa roho mbaya kama hizo za kutukana wanawake wenzenu ambao hawajawakosea kitu mtaishia kubakwa tu…..Mnajitiaga nuksi wenyewe.”
10.                        KUHUSU  WANAUME  WAKIZUNGU: Mange Kimambi  anasema  usimjudge  mwanaume  wa kizungu  kwa kumwangalia tu.
“ Au issue ni kuolewa na mzungu? mmemsema mzungu wa watu choka mbaya sijui nini? hata kama si wake yeye, nyie umaskini wa huyo mzungu unawahusu nini? na wazungu hamuwajui nyie anaweza tembea na soksi zimetoboka kwenye account ana mamilinion….. usim judge mzungu kwa mavazi hata siku moja “

 

Copyright © 2013. UBUYU KITAANI - Haki zote zimehifadhiwa
Template Modify by Habarizetuleo TEAM
Proudly powered by MAN DUGX